Kukulia kwenye nyumba isiyokuwa na baba wa kutegemewa na yenye mama anayekunyanyasa kihisia, ilikuwa rahisi kwa Tom Stewart kuingia kwenye mtego wa kundi la watu wabaya. Huku akizoea desturi ya kufuata ushawishi wa wengine na kutaka uthibitisho kutoka kwa wakubwa wake, Tom alijikuta amenaswa kwenye mwongo wa dhuluma kutoka kwa kiongozi wa kikundi chake cha Maskauti.
Kiwewe cha utoto wake kuharibiwa kinamfuata hadi siku za baadaye, ambapo anakumbana na majaribu si haba. Kupitia janga la kiafya, mahusiano yaliyovunjika na kifo cha mtoto wake wa kiume, Tom anashikilia imani yake isiotetereka. Wakati kesi muhimu inapomweka kwenye barabara ndefu ya msamaha na uponyaji, Tom anaanza kuona kusudi la Mungu kwenye uchungu aliokuwa akiupitia. Badala ya kusalia kwenye uchungu, Tom anakabili siku zake za nyuma, akithibitisha kuwa hata katika hali mbaya, Mungu anaweza kugeuza mabaya kuwa mema.
Katika kitabu chake cha kumbukumbu ya kuhuzunisha, Tom anawasilisha ujumbe wa tumaini katika mazingira ya madhara yasiyofikirika. Kupaa Kama Tai ni hadithi ya uvumilivu na nguvu ya msamaha, inayotukumbusha kuwa kutokana na neema ya Mungu, kuna uwezekano wa kuinuliwa juu zaidi ya hali zetu za kupondeka.
"Katika utoto wake wote, Tom Stewart alikumbana na mwongo mzima wa dhuluma ya kingono kutoka kwa kiongozi wa kikundi chake cha Maskauti Wavulana. Katika kitabu chake dhahiri, Kupaa Kama Tai, anatusimulia siyo tu kisa chake, bali pia anampatia msomaji maarifa ya kutambua ishara za dhuluma na kutoa njia ya uponyaji kupitia imani katika Yesu. Kitabu hiki lazima kisomwe na kila mzazi ili kumsaidia kuwalinda watoto wake na vilevile lazima kisomwe na kila mtu aliyeteseka kama Tom alivyoteseka."- Josh D. McDowell, Mwandishi